NGUVU YA ROHO YENYE UZIMA
NGUVU YA ROHO YENYE UZIMA Mithali 18:14 "Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake; Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?" Andiko hili linaeleza ukweli mzito wa maisha: nguvu ya kweli ya mwanadamu haimo katika mwili, bali rohoni. Mtu mwenye roho imara anaweza kuvumilia magonjwa, huzuni, au hata upweke. Lakini mtu aliyekata tamaa rohoni, hata akiwa na afya, hawezi kusimama. 1. Roho Imara ni ngome wakati wa shida Katika 2 Wakorintho 4:16, Paulo anaandika: "Kwa hiyo hatulegei; hata ijapokuwa utu wetu wa nje unaharibika, lakini utu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku." Hii inaonyesha kuwa nguvu ya ndani – ya kiroho – ndiyo inayotufanya tusivunjike hata tukikabiliwa na taabu. 2. Roho iliyovunjika ni hatari zaidi ya ugonjwa wa mwili Kuvunjika kwa roho ni hali ya mtu kupoteza matumaini, kupoteza kusudi, na kuhisi kana kwamba hakuna tena tumaini la kesho. Zaburi 34:18 inasema: "Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, Huwaokoa waliopondeka roho." Hii ni ah...