IMANI NI NINI?
Imani ni Nini?
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."
(Waebrania 11:1)
Imani ni msingi wa maisha ya Kikristo. Bila imani, hatuwezi kumpendeza Mungu. Imani ni kukubali na kuamini kile Mungu amesema hata kama bado hujakiona kwa macho.
Imani ya kweli inajionyesha kwa:
Kumtumainia Mungu katika kila hali
Kutii Neno la Mungu bila masharti
Kuishi kwa matumaini hata katikati ya giza
Mfano hai:
Ibrahim alimwamini Mungu hata wakati hakuwa na mtoto, na Mungu alimbariki kwa mtoto wa ahadi – Isaka.
Mafunzo ya Leo:
1. Imani ni zawadi kutoka kwa Mungu. (Warumi 12:3)
2. Imani huja kwa kusikia Neno la Mungu. (Warumi 10:17)
3. Imani hutenda kazi kwa upendo. (Wagalatia 5:6)
Swali la Kutafakari:
Je, ninaamini nini kuhusu Mungu leo? Naamini anajua shida zangu? Anaweza kunisaidia?
Omba Nasi:
> Ee Bwana, ongeza ndani yangu imani ya kweli. Nisadie kukuamini hata nisipoona. Amina.
Maoni
Chapisha Maoni