KWANINI NIOGOPE SIKU ZA UOVU?
KWANINI NIOGOPE SIKU ZA UOVU?
Andiko Makuu: Zaburi 49:5
"Kwa nini niogope siku za uovu, ubaya ukinizunguka miguuni pangu?"
Ufafanuzi Mfupi:
Mwandishi wa Zaburi anaonyesha ujasiri mkubwa wa kiroho. Anauliza swali la kutafakari: Kwa nini niogope?
Ni wazi kuwa anaelewa jambo moja kuu — kwamba Mungu ndiye ngome yake hata siku za giza. Siku za uovu hazimaanishi Mungu hayupo. Zina maana kuwa IMANI yetu ndiyo inapimwa.
Hofu huja tunapotazama mazingira, lakini AMANI huja tunapomtazama Mungu.
Maandiko ya Kuimarisha Ujumbe:
1. Isaya 41:10
"Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia; nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu."
2. Zaburi 23:4
"Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na gongo lako vyanifariji."
3. Warumi 8:31
"Basi, tuseme nini juu ya hayo? Ikiwa Mungu yu upande wetu, ni nani aliye juu yetu?"
Hitimisho la Somo:
Siku za uovu zitaibuka — huja kwa kila mmoja wetu. Lakini usiogope. Ukimtazama Mungu, utaona kuwa huna sababu ya kuishi kwa hofu. Uovu ukikuzunguka, Mungu yuko ndani yako. Na aliye ndani yako ni mkuu kuliko yote!
Imeandaliwa na:
Kisakenyi Mnzava
Mhubiri na Mwalimu wa Neno la Mungu
Mawasiliano:
WhatsApp/Simu: +255 764 317 590
Email: issacklucas2@gmail.com
#SomoLaImani #Usiogope #Zaburi49 #NenoLaMungu #UjumbeWaAsubuhi #MunguYupo

Maoni
Chapisha Maoni