DALILI ZA KUJA KWA KRISTO NA MWISHO WA DUNIA – JE, UMEJIANDAA?
DALILI ZA KUJA KWA KRISTO NA MWISHO WA DUNIA – JE, UMEJIANDAA?
MAANDIKO (Mathayo 24:3-14):
Yesu alikaa juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani wakisema:
"Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?"
(Mathayo 24:3)
Yesu aliwajibu:
"Angalieni, mtu asiwadanganye. Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi." (aya 4-5)
"Mtasikia vita na matetesi ya vita... lakini mwisho bado." (aya 6)
"Kutakuwa na njaa, tauni, na matetemeko ya ardhi mahali mbalimbali. Lakini hayo yote ni mwanzo wa utungu." (aya 7-8)
Waumini watachukiwa, kusalitiwa, na kuuawa. (aya 9-10)
"Manabii wa uongo watatokea... upendo wa wengi utapoa." (aya 11-12)
"Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka." (aya 13)
"Tena habari njema ya Ufalme itahubiriwa duniani kote; ndipo ule mwisho utakapokuja." (aya 14)
UJUMBE WA KUTAFAKARI:
Je, dalili hizi hatuzioni leo? Vita, tauni, vifo, njaa, chuki, na upendo wa kweli kupoa? Huu ni wakati wa kumrudia Yesu, kuwa macho, na kueneza injili. Usingoje hadi mwisho ufike — jiandae sasa.
#YESUANAKUJA #MWISHOWANYAKATI #MATHAYO24 #INJILIYAKWELI #IMANINATUMAINI #BIBILIA
Imeandaliwa na: Kisakenyi Mnzava
Mwalimu wa Neno la Mungu na Mshauri wa Mahusiano
Pata mafundisho zaidi kupitia:
Facebook/TikTok/Instagram
Email: Issacklucas2@gmail.com
WhatsApp: +255 764 317 590
Maoni
Chapisha Maoni